Mpambano wa kugombea kiti cha udiwani kata ya Njombe mjini unafikia tamati kesho kutwa kwa wananchi wa Njombe kuamua wanamtaka nani awe diwani wao baada ya kifo cha Jackies.
Mpambano huo uliokuwa wa kukamiana ulijaa vituko na matukio mbalimbali ikiwapo polisi kupigwa na wafuasi wa CCM, wafuasi wa CDM kushitakiwa mahakamani kwa kuwashambulia wana CCM na kumtishia maisha Jah People na vijembe mbalimbali visivyoandikika.
Vyama vyote vinasemekana vimeleta wabunge kutoka sehemu mbalimbali kuongeza nguvu ambapo CDM wamemleta David Silinde wa Mbozi wakati CCM wamewaleta John Nchimbi wa Songea, Deo Sanga, Deo Filikunjombe wa Ludewa, Kayombo wa Mbinga na Pindi Chana naibu Waziri wa Jinsia na Watoto.
Mpambano huo utahitimishwa kwa mikutano mikubwa itakayofanyika Jumamosi sehemu mbalimbali za mji wa Njombe.